Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kendrick Lamar, Drake: Vita ya muziki iliyoleta mafanikio makubwa ya nyimbo za diss

Kendrick Lamar, Drake Kendrick Lamar na Drake.

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miezi ya hivi karibuni, tofauti kati ya Kendrick Lamar na Drake zilichukua attention kubwa, zikionyesha mvutano mkubwa ndani ya ulimwengu wa muziki wa hip-hop. Wawili hao walitambiana kwa mfululizo wa nyimbo kadhaa, huku myimbo za Kendrick Lamar zikifanikiwa sana kwenye chati za muziki.

Nyimbo za Kendrick Lamar zilizolenga kumdiss Drake zilipata mafanikio makubwa kwenye chati za muziki. Wimbo wa “Not Like Us” uliingia moja kwa moja kwenye nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100, ukiashiria nguvu ya mashabiki wa Kendrick na ubora wa kazi yake.

“Euphoria,” wimbo mwingine wa diss, ulipanda hadi nafasi ya tatu kwenye chati hiyo hiyo, ukithibitisha kuwa mashabiki walikuwa wakisikiliza kwa makini kila neno alilosema.

Mvutano kati ya Kendrick Lamar na Drake ulianza mapema mwaka huu baada ya Kendrick Lamar kushirikishwa kwenye wimbo wa Future na Metro Boomin, “Like That,” ambapo Kendrick alimkejeli Drake kwa kujitaja kuwa yeye ni bora zaidi na kumpinga kuwa sehemu ya “big three” ya wanamuziki wakubwa wa hip-hop pamoja na J. Cole. Hii ilisababisha majibizano makali ambapo Drake alijibu na nyimbo kama “Push Ups” na “Taylor Made Freestyle,” akimshambulia Kendrick Lamar kulingana na tabia zake.

Kufikia Mei 2024, vita hii ilifikia kilele chake wakati ambao Kendrick alikuwa ametoa wimbo “Not Like Us,” ambao artwork yake ilionyesha ramani ya nyumba ya Drake. Hatua hii ilisababisha shambulio la risasi kwa mlinzi wa Drake huko Toronto. Katika kujibu, Drake aliachia wimbo “The Heart Part 6,” akiwa na nia ya kuendeleza bifu yao.

Mwishoni mwa mwezi Mei, Anthony Tiffith, mwanzilishi wa lebo ya Top Dawg Entertainment, alitangaza kuwa mzozo huo umemalizika na kusifia wasanii hao kwa kuuweka mzozo huo kwenye muziki pekee, bila kushambuliana mwilini. Aliongeza kuwa lebo hiyo ina mpango wa kutoa albamu ya kusherehekea miaka 20 ya TDE, Kendrick Lamar akiwa msanii Bora wa muda wote chini ya Lebo hiyo.

Kwa sasa, ingawa vita vya maneno vimepungua, bado kuna uwezekano wa majibizano mapya kuibuka, hasa ikizingatiwa maneno ya Drake kwenye mitandao ya kijamii, akidokeza kuwa anaweza kurudi kwenye muziki wa majibizano wakati wowote.

Kwa kuzingatia historia ndefu ya mvutano kati ya wasanii hawa wawili, mashabiki na wadau wa muziki wa hip-hop wanaendelea kufuatilia kwa karibu matukio yajayo katika vita hii ya kisanii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live