Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kelly Haso alivyochomoza kutoka Buza mpaka Bogos

46992 Pic+kelly

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kelly Haso ni mwanamuziki wa Bendi ya Bogos Musica iliyopo chini ya Rais Nyoshi Elsaadat, ambaye ameamua kujitosa kwenye muziki kufuata nyayo za mkali Fally Ipupa.

Ndoto zake hizi ni za miaka mingi tangu akiwa amemaliza kidato cha nne ambapo alianza kwa kuwambia marafiki zake nyimbo za nyimbo mkali huyo ikiwemo Associe, Kiname, Mungala, Bafana na nyingnezo.

Katika harakati hizo, hakuishia hapo kwani amewahi kushiriki mashindano mbalimbali ikiwemo ya Club Rahaleo shoo msimu wa tatu japokuwa hakufanikiwa kushinda ila alipata bahati ya zari la kuchukuliwa na Menejimenti ya Nyegerawaitu iliyoko Buza inayosimamiwa na Dr Ntambanamungu.

Wakati akiwa kwa Nyegerawaitu alifanikiwa kutoa nyimbo ‘Natamani’ na kupata shoo za hapa na pale hadi alipoachana nao na kwenda kujiunga na bendi ya Bogos Musica chini ya Nyoshi Elsaadat.

Ilikuwaje akaingia Bogoss Musica kwa Nyoshi?

“Mimi nilianza kumfahamu Nyoshi El Saadat toka akiwa bendi ya Fm Academia,mwanzo nilikuwa tu namsikia Nyoshi.

“Kuna siku bendi ya Fm Academia ilikuja kupiga Yombo kwenye ukumbi wa Jimmy Agent, nilienda lakini niliishia nje, hivyo ikawa kila wakipiga mimi naishia nje, hadi hapo siku moja pale nilipokutana na mwanamuziki 33 kabla hajaondoka Fm Academia na kumwambia mimi ni muimbaji.

“Mwanamuziki huyo katika kunijaribu kama naweza kuimba, alinitaka nimwimbie ndipo nilipoimba wimbo wa Fally Ipupa wa Associe, akanisifu na kuniomba tubadilishane namba,”anasema.

Baada ya muda kupita Kelly Haso anasema siku moja akiwa nyumbani aliona namba ya 33 ikimpigia na kumtaka aende nyumbani kwake Mwananyamala Komakoma.

Walipoamaliza maongezi waliongozana naye hadi kwenye mazoezi ya Fm Academia yalikuwa yanafanyika Msasani Club kipindi hicho na kumtambulisha kwa Nyoshi na hapo ndipo alipomfahamu kwa kumuona ana kwa ana kwa mara ya kwanza.

Naye kama ilivyokuwa kwa 33, alimataka amwimbie wimbo wa Fally Ipupa wa Kiname na Associe na baada ya kumsikiliza alimwambia anajitahidi ila aendelee kufanya mazoezi, kisha wakapeana namba na kuahidi kunitafuta.

“Baadaya hapo nikawa mimi ndio namsumbua sana Nyoshi, kwani yeye alikuwa bize, nikawa namtumia voice ninavyoimba, akawa ananijibu kuwa najitahidi ila niendelee kufanya mazoezi, Nyoshi akawa ananifundisha kwa njia ya simu tu, kwani alikuwa ananipa maelekezo ya kuniambia nifanye mazoezi ya pushapu, kukimbia ili niwe na pumzi.

“Hata alipoamua kuanzisha Bendi ya Bogoss, nikawa naendelea kumtumia voice (sauti) na mwisho wa siku akaniita nyumbani kwake Sinza akanifanyie interview na baada ya hapo ndipo akanichukua rasmi kutumikia bendi hiyo,”anasema Haso.

Atoa wimbo wake

Hata hivyo, pamoja na kuwa Bogoss Musica , Kelly Haso ametoa wimbo wake nje ya Bendi alioupa jina la ‘Comeback’.

“Wimbo huu una mahadhi ya Rhumba, nimetengeneza katika studio ya Soft Record huku mtayarishaji akiwa Pitshou Mechant.

“Pia nimeuandika mwenyewe na kupigwa gitaa la base na Dekanto Bezi huku gitaa la solo akiwa amepiga Pitshou,” anaeleza.



Chanzo: mwananchi.co.tz