Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Kazi yangu inahusu kuosha meno ya maiti - Filinda

Filinda Kazi yangu inahusu kuosha meno ya maiti - Filinda

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Filinda Kamau ni Mkenya kutoka Kaunti ya Nakuru na amejikuta kuwa mwanamke maarufu mtandaoni kwa kushiriki video za TikTok akionyesha hasa kazi zake kutoka katika chumba kimoja cha kuhifadhia maiti huko Nakuru, ambako anafanya kazi kama mhudumu wa kuosha na kutayarisha maiti.

Filinda anasema anataka kuwasaidia watu kukomesha na hofu ya vyumba vya kuhifadhia maiti na kumaliza unyanyapaa kwa watu wanaofanya kazi katika maeneo hayo.

Mwanadada huyu ni maarufu kwani anasimulia kazi zake katoka mochari, na anashirikisha wafuasi wake katika uzoefu huo wa wa jinsi ya kusitiri na kushughulika miili ya wafu hadi wakati wanapozikwa.

“Mojawapo wa sababu zangu kuweka kazi zangu nikiwa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye mitandao ni kwasababu kuna dhana potofu mno kuhusu watu kama mimi ambao ni wahudumu wa mochari , kama watu wachafu au ambao hawana akili timamu , ila ukweli ni kuwa wengi wetu tumesomea kazi hii ”anasema Filinda

Kwa kiasi kikubwa dhana kuhusu shughuli za kuwapa buriani wafu barani Afrika , zimezingirwa na uoga na hofu hadi kiasi fulani hivyo basi mwanadada huyu anasema kuwa ni muhimu watu kuelewa kwa undani kuhusu kazi za wahudumu wa vyumba vya kuhifadhia maiti.

Je nini kilichochea Filinda kupenda kazi ya mochwari Mwanadada huyu anasema kuwa akiwa shule ya sekondari alikuwa na ndoto ya kuwa daktari na alipokamilisha masomo ya sekondari alipata matokeo ambayo yangemuwezesha kusomea udaktari ila hali ya kifedha nyumbani kwao ilikuwa haijakaa sawa hivyo basi ilibidi atafute kozi ambazo familia yake ingeweza kugharamia.

Chaguo lake kufanya Kozi ya kwanza katika sekta ya Afya ni ( Mortality Science) au muhudumu wa maiti, alisomea katika chuo kikuu cha Nairobi na kupata shahada.

Ni hali ambayo jamii yake ilichukua muda kukubali kwani walishangaa ni kwanini mwanadada kama yeyealikubali kufanya kazi katika mojawapo ya vyumba hospitalini vinavyoogopwa sana .

Ila Filinda alipiga moyo konde na kukubali kusomea mengi kuhusiana na jinsi ya kushughulikia wafu na matayarisho ya mwisho ya kuiaga miili ya watu.

“Mimi nikiamka asubuhi, naomba Mungu sana ili anilinde sana wakati nikiwa mochari, hii kazi sio ya watu ambao ni waoga' anasema Filinda Filinda ni mke na mama, anafurahi kuwa mume wake alikubali kazi anazofanya, japo kwa baadhi ya marafiki na jamaa wa karibu walimtoroka kwa kuhofia kazi ambazo anazifanya kila siku kwenye mochari.

Akiwa sasa anaelekea kutimia miaka 26, amefanya kazi hii kwa miaka 9 na anasema kuwa ameikubali na kwake hajaona cha kuhofisha.

Je kazi za kila siku kama mhudumu wa mochwari ni zipi? Filinda anasema kuwa kazi zake zinahusu wafu, kuhakikisha kuwa mwili wa mtu ambaye amefariki umepokewa kwa utaratibu ambao unafaa, kupokea mwili kutoka kwa familia au maofisaa wa usalama, kuuosha, kusugua meno, kuhakikisha kuwa muonekano wake uko sasa kwa mfano macho na mdomo yamefungwa.

Uzoefu wake hasa siku za kwanza alipoanza kazi hii alikuwa na hofu na uoga, kwani ilikuwa wakati alianza kuona miili ya watu ambao wamefariki, mara kwa mara alikuwa anajiuliza “na je nikaanza kuhudumia mwili alafu alafu ghafla uanze kunisemesha nitafanya vipi” Mambo kama hayo yalipita kwenye akili yake, vile vile alikuwa na hofu ya kusalia peke yake hasa katika cumba chenye barafu ya kuhifadhi miili (cold room) pekee yake lakini kwa sasa na uzoefu alionao hana hofu hata kidogo.

Kwa kawaida kwenye sekta hii ni wanaume wametambulika kuifanya, ila mwanadada huyu anasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni wanawake pia wanapiga moyo konde na kujitosa kwenye vyumba va kuhifhadhia maiti kufanya kazi huko kupata riziki .Ila Filinda anasema kuwa ameona wanafunzi wengi wakitamani kufanya kazi lakini wanaachia katikati kwasababu ya hofu.

Anapoulizwa ikiwa anakuwa na ndot za ajabu au hofu baada ya kufanya kazi anasema kuwa amejifunza kuacha maswala yanayohusu kazi huko , naanapoingia nyumbani kwake anavalia kofia ya mke na mama.

Changamto kubwa katika kazi yake, inakuwa ni wakati anapokea mwili wa mtoto mdogo, kwake yeye anaona vigumu kuvalisha na kuosha mtoto wakati yeye ni mama wa mtoto mdogo.

Pia wakati mmoja akiwa anafanya kazi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Nakuru alipokea miili ya watu waliofariki kutokana na ajali ya barabarani kama kawaida yake Filinda anasema kuwa akipokea maiti huweka kando mwili kwa saa hata mbili ili kuhakikisha kuwa mtu huyo kweli amekata roho.

Mwanadada huyu anasema kuwa alihisi kana kwamba mtu mmoja kati yao alikuwa hai na aliishia kukimbia mbio.

Ni mojawapo wa changamoto ambazo anasema zipo katika kazi yoyote. Katika kuhimiza wanawake kutochagua kazi zozote anasema kwamba, nafasi za kazi huenda sio nyingi lakini mtu anaweza kuangazia sekta nyenginezo ambazo watu wanakumbwa na itikadi au imani potofu hivyo basi kukosa kuzipa uzingativu na hapo ndipo pana fursa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live