Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya mume wa Vera Sidika baada ya mkewe kung'oa makalio bandia

Vera Sidika Mume Kauli ya mume wa Vera Sidika baada ya mkewe kung'oa makalio bandia

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa muziki toka Kenya, Brown Mauzo yeye kwake umbo la kuvunja chaga sio inshu, ameeleza kwamba atampenda zaidi mke wake Vera Sidika na muonekano huu alionao hivi sasa tofauti na mwanzo.

@brownmauzo254 amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku moja imepita baada ya mkewe Vera Sidika kuweka wazi kufanyiwa upasuaji na kupunguza sehemu kubwa ya makalio yake baada ya kuona anapata matatizo ya kiafya.

Wawili hao ambao ni wazazi kwa mtoto mmoja wa kike, jina Asia, walikuwa pamoja katika mchakato wa upasuaji mpaka kukamilika. Brown Ameeleza. Pia amedai kulimiss umbo la awali la mkewe ila anachokipenda kutoka kwa Vera ni moyo wake.

Aidha, @queenveebosset yeye kupitia ukurasa wake wa Instagram, amewashauri wadada ambao wanampango wa kuongeza sehemu zao za mwili basi wasifanye hivyo kwani itawaletea matatizo kwa siku za usoni. Pia ameahidi kuonyesha video za tukio zima la kufanyiwa upasuaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live