Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Vera Sidika baada ya kung'oa makalio ya mchongo

Vera Sidika Mdqw Kauli ya Vera Sidika baada ya kung'oa makalio ya mchongo

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Vera Sidika amesema kuwa amefanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio yake na hata kuchapisha mtandaoni picha iliyoonyesha mabadiliko yake na muonekano wake wa sasa baada ya kuondoa makalio ya bandia.

Sidika alisema kuwa ilibidi afanyiwe upasuaji huo kwa kuwa upasuaji wa kuubadilisha mwili wake umemletea shida baadaye ikiwemo shida ya kiafya.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliongeza na kusema kuwa safari hiyo ya kubadilisha mwili wake uwe kama ulivyokuwa sasa haijakuwa hatua rahisi huku akiwashauri wanadada ambao wangetaka kufanyiwa upasuaji wa kimwili kuukubali mwili wao na kubaki walivyo kwani itawaletea shida huko mbeleni.

"Wanadada tafadhalini, mjue kujipenda mlivyo na msikubali shinikizo la rika liwafanye mkimbilie kufanya mambo ambayo yatawaharibia maisha yenu huko mbeleni.

“Wanawake, tafadhali jifunzeni kujipenda na kamwe msijaribu kuruhusu shinikizo la ujana liwaharakishe katika mambo yatakayo waletea madhara baadae. Nimebahatika kuwa hai, Mungu ananipenda sana," alisema Vera.

Sidika alisema kuwa yalikuwa maajabu na kuwa alikuwa na bahati kuwa hai baada ya mwili huo wake wa zamani kumleta shida ya kiafya.

"Nina bahati kuwa hai. Sikusherehekea siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu, lakini tuko hapa sasa. Heri ya kuzaliwa kwangu. Nimekuja kushukuru kuwa na uhai na kutoyachukulia mambo yoyote hivihivi," alisema Vera.

Alisema kuwa mambo hayakuwa rahisi kabla aende kwenye upasuaji wake na hata alipoenda alimshukuru Mungu kwa kumpa zawadi ya uhai na afya njema.

Mjasiriamali huyo aliongeza kuwa amejikubali alivyo na amejifunza kuizoea hali hiyo ya mwili wake mpya na hata nini itendeke ataendelea kujipenda alivyo sasa.

Hii imetendeka baada ya siku yake ya kuzaliwa kupita hivi majuzi na mwanasosholaiti huyo kusherehekea kuwa kuzaliwa upya.

Vera amesema mashabiki wake kuwa bado yeye wa sasa hivi ni yule yule Sidika aliye mzuri na hajabadilika kivyovyote vile.

Sidika aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kumwonyesha upendo na aliwahimiza wamsaidie kwa safari hii yake mpya.

"Naishukuru familia yangu haswa mume wangu kwa kuwa na mimi kwa wakati huu mgumu, na hata nyinyi mashabiki wangu," alisema.

Alisema ataanika mtandaoni video za upasuaji wake ili kuweza kuwashinikiza wale ambao wangetaka kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha mwili wao wasijaribu kufanya hilo.

“Huu umekuwa wakati ngumu zaidi maishani mwangu, kwa sababu ya hatari na matatizo ya kiafya, ilinibidi kufanyiwa upasuaji. Bado siamini lakini nimekubali na nimejifunza kujipenda bila kujali.

“Kusema kweli Imekuwa ngumu sana, hata sikusherehekea siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu, lakini hapa tumefika. Heri ya kuzaliwa kwangu.

“Mimi Mpya nimekuja kuthamini maisha na kamwe sichukulii mambo kawaida. Asante kwa familia yangu, haswa mume wangu kwa kunisaidia.

“Kwa mashabiki wangu Mimi bado ni yule yule Vera Sidika mtamu na hilo halijabadilika. Nakushukuru kwa upendo, support na maombi tukipitia safari hii pamoja nami.

“Nitakuwa nikiweka video zangu za safari yangu ya upasuaji hapa, kwa wale ambao wamekuwa wakifikiria kupata upasuaji au kubadilisha chochote kwenye miili yao hii inaweza kubadilisha mawazo yenu.” Vera Sidika via Instagram.

"Kuzaliwa upya, hii imekuwa awamu ngumu zaidi maishani mwangu kwa sababu ya hatari na matatizo ya kiafya, ilinibidi kufanyiwa upasuaji. Nimekubali na nimejifunza kujipenda bila kujali.

"Nitakuwa nikiweka video zangu za safari ya upasuaji hapa, kwa wale ambao wamekuwa wakifikiria kupata upasuaji wa nyara au kubadilisha chochote kwenye miili yao hii inaweza kubadilisha mawazo yako,” amesema Vera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live