Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Diamond baada ya kushinda tuzo ya MTV

Diamond Mssa(1) Kauli ya Diamond baada ya kushinda tuzo ya MTV

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Diamond Platnumz ameshukuru Mungu baada ya kutuzwa kama msanii bora Afrika kwenye tuzo za MTV EMA mwaka huu.

Kwenye kauli yake Diamond alishukuru baraza lake muziki kwa bidii yao ambayo imefanikisha ushindi huo kwa ushirikiano mwema na juhudi za kila mmoja.

"Nasifu sana baraza langu la muziki kwa bidii,tumebadilisha muziki wa Tanzania kuwa Bora zaidi barani Afrika Sifa ni kwetu wote,"alisema.

Kwenye taarifa yake Diamond alipongeza Rais wa Tanzania kwa bidii zake kuhakikisha wasanii wanapata mazingira mazuri ya kufanya sanaa bila tatizo.

Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Jumapili, Diamond aliibuka kama msanii bora wa Afrika, (Best African Act).

Diamond alikuwa anamenyana na wasanii kama vile Burna Boy, Asake, wote kutoka Nigeria na mrembo chipukizi kutoka Cameroon, Libianca pamoja na Tyler ICU.

Msanii huyo amefanya urejeo wake kwenye tuzo za MTV EMA mwaka huu kuwa kubwa Zaidi baada ya kuwabwaga wasanii wakubwa barani Afrika kushinda tuzo hiyo kwa mara ya pili katika historia ya maisha yake ya muziki.

Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika na mwimbaji Bora kwenye MTV EMA 2015.

Hafla ya tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Paris Nord Villepinte, nchini Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live