Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Basata akumbushia ugomvi wa Rayvanny na Diamond

Katibu Basata Akumbushia Ugomvi Wa Rayvanny Na Diamond Katibu Basata akumbushia ugomvi wa Rayvanny na Diamond

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Rayvanny tayari amewasili nchini kutoka Kenya ambapo alienda kwenye hafla ya utolewaji tuzo za East Africa Arts Entertainment Awards 2024 (EAEA) ambapo ameondoka na tuzo tano.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dkt. Kedmon Mapana, akiwa katika mapokezi ya msanii huyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere amesema kuwa alipoingia kazini mwaka 2022 kazi ya kwanza aliyokabidhiwa ni kutatua kesi ya Rayvanny na Diamond.

"Tunampongeza sana, watu wengi hawafahamu Rayvanny mimi ni kijana wangu, nilipoingia kazini Julai 12, 2022, kazi ya kwanza niliyokabidhiwa na mheshimiwa waziri wa wakati huo ni kumaliza kesi ya Diamond na Rayvanny, hiyo ndiyo ilikuwa kazi yangu ya kwanza Basata kwa hiyo lazima niikumbuke lakini nashukuru sana Mungu kwamba nilipambana ile kazi iliisha vizuri na vijana wangu walipatana na wakarekdi ngoma," amesema Mapana.

Katika tuzo hizo ambazo Rayvanny amerudi nazo nchini ni tuzo ya Msanii Bora wa Kiume (East Africa), Album/EP bora (East Africa), Mwandishi bora (East Africa), Best lovers’ choice single (East Africa), Best inspirational single (East Africa).

Aidha kwa upande wake Rayvanny akizungumza na waandishi wa habari alipowasili nchini amegusia suala la Harmonize na Diamond kupatana na kuishi kwa amani.

"Mimi ni mtu ninayependa kuweka sana amani pasiwe na ugomvi na vita kama ambavyo mimi nimetoka Wasafi changamoto zilikuwa nyingi lakini tumeweza kuitunza amani na maisha mengine yanaendelea sababu mtu mwingine anajua labda zikishatoka hela unanuna lakini mwisho tunafanya kazi tunafanya biashara familia lazima iendelee pia mimi nilikuwa na kila sababu ya kusema kwamba tunaweza kugombana lakini tuliweza kuitunza amani kwa hiyo nikamwambia pia sioni kama kuna faida yoyote ya kuendelea kugombana nafikiri Harmonize ameongea sana na Diamond kuwa maisha mengine yaendelee," amesema.

Hata hivyo, kuhusiana na baadhi ya watu wanaodai kuwa kupatana kwa wasanii hao kunaweza kupunguza ushindani wa kimuziki Rayvanny amesema ushindani wa gemu hauwezi kupungua kwani kila mmoja ataendelea kutoa ngoma zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live