Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kasisi aasi Kanisa Katoliki na kuoa

Screenshot 20231022 201748 Opera News Kasisi aasi Kanisa Katoliki na kuoa

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki katika Kaunti ya Kiambu, Bw Edwin Gathang’i, amefunga ndoa na rafikiye mwanamke wa muda mrefu.

Bw Gathang’i alifanya harusi na Bi Margaret Wanjira katika Uwanja wa Michael’s Pot, eneo la Ikinu, Githunguri. Bwana harusi aliasi kanuni za Kanisa Katoliki, ambazo huwa haziwaruhusu makasisi kuwa na mahusiano ya kimapenzi au kuwa na familia.

Bw Gathang’i aliiambia Taifa Jumapili kwamba hangeweza kujificha ndani ya kanuni hizo kali za kanisa, wakati moyo wake ulihitaji kuwa na mke.

“Niliona niache kujificha. Nilimpenda Bi Wanjira kwa muda mrefu na nikaamua kufuata kile moyo wangu ulipenda. Harusi yangu ilishuhudiwa na makaasisi wengi. Huu ni mwanzo mpya kwa wale ambao wanataka kuwa familia kujiunga nasi,” alisema Kasisi Gathang’i.

“Namshukuru mke wangu kwa kukubali awe nami daima. Alikubali niwe mume na baba wa watoto wake. Kasisi anaweza kuwa na familia na pia  atekeleze majukumu ya kanisa,” aliongezea.

Bw Gathang’i alifanya uamuzi wa kujiunga na Kanisa la Kikatoliki  la Charismatic, lililo na sheria inayoruhusu makaasisi kuwa na mke au familia. Ameishi katika maeneo ya Amerika Kusini na Kaskazini.

Kaasisi huyo alipata mafunzo kwenye Kanisa la Kikatoliki la Kirumi, lenye msimamo na sheria kali inayozuia makaasisi kuwa na familia.

Bi Wanjira, aliyezungumza na Taifa Jumapili, alimtaja Bw Gathang’i kuwa mwenye ujasiri kwa kufunga ndoa naye.

“Mungu hakufanya makosa kuumba mume na mke. Kuna sheria inayoruhusu kuwepo kwa ndoa. Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu na kuonelea tusiendelee kujificha,” akasema Bi Wanjira.

Gathang’i aliiambia Taifa Jumapili kwamba ataendelea kutekeleza majukumu ya kanisa na kuwalea wanawe wawili. Gachagua sasa aomba mwafaka na mabroka wa kahawa ili...

Chanzo: www.tanzaniaweb.live