Rapa wa Marekani Kanye West, amemeki heading katika mitandao ya kijamii mara baada ya kumpokonya mwandishi wa TMZ simu kufuatia swali alilomuuliza kuhusu uhuru wa mke wake Bianca Censori kwenye mitandao ya kijamii.
Kanye alikonekana kukasirika na swali hilo ndipo akachukua simu ya mwandishi huyo takribani dakika 3, huku akizungumza naye kwa ukali mambo kadhaa wa kadhaa kuhusu yeye kufuatiliwa katika mambo yasiyo ya msingi huku kuna mengi mazuri ambayo anafanya na ahojiwi kuhusu mambo hayo.
Aidha katika mazungumzo hayo Kanye ametoa ofa kwa mwandishi huyo kufanya naye kazi huku akimuahidi kumpatia mshahara mara mbili ya kile anacholipwa.
Kwa mujibu wa TMZ, ripota wao ameikataa ofa ya Kanye West ya kufanya naye kazi.