Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye afungiwa Instagram, amuwaki Mark Zuckerberg, Elon Musk amkaribisha Twitter

Kanye Zuckerberg .jpeg Kanye afungiwa Instagram, amuwaki Mark Zuckerberg, Elon Musk amkaribisha Twitter

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtandao wa Instagram umemfungia Kanye West kupost au kufanya lolote lile kwenye ukurasa wake wa mtandao huo.

Aidha msemaji wa META amekiri kufanya usimamishaji wa muda wa account ya rapa huyo bila kuweka bayana ni post ipi hasa iliyo pelekea Rapa huyo kufungiwa.

Kanye amerudi rasmi twitter toka afanye hivyo November 2020 na kumshushia lawama mmiliki wa META (Facebook, Instagram pamoja na WhatsApp) Mark Zuckerberg kwa kumuondoa Instagram wakati walizoea kuwa washkaji.

Kwenye tweet hiyo ya Ye, Tajiri Namba moja duniani, Elon Musk amecomment akimkaribisha rafiki yake huyo kwa kurudi tena twitter baada ya kipindi kirefu.

Ye amekuwa kwenye matukio ya kurushiana maneno na watu mbalimbali kwenye mtandao wake wa Instagram baada tu ya kuzindua T Shirt zake za WHITE LIVES MATTER kwenye Yeezy Fashion Show Jumatatu hii ya Oktoba 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live