Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye achekelea penzi la Kim na Davison kuvunjika, atupa dongo

Kim Kanye Davidson Kanye achekelea penzi la Kim na Davison kuvunjika

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku chache baada ya supastaa Kim Kardashian na mpenzi wake Pete Davdison kuachana, aliyekuwa mume wa Kim, rapa Kanye west ameibuka kwenye mtandao wa Instagram na kusherehekea kuvunjia kwa penzi hilo. Kanye aliposti ukurasa feki wa mbele wa gazeti la The New York Times lenye headline inayosomeka, “Skete Davidson Dead at Age 28.”

Chini ya picha hiyo, Kanye aliandika maneno, “Kid Cudi yeye akimaanisha unachezea mazishi lakini unaogopa kupondwa chupa.”

Rapa Kid Cudi, ni rafiki mkubwa wa Davidson ambaye anadaiwa kuwa sababu kubwa ya makasiriko ya Ye, aliondoka kwenye stage wakati wa kupafomu mara baada ya kurushiwa chupa katika tamasha lake huko Rolling Loud Miami mwezi uliopita.

Cudi aliingia n akum-replace Ye kwenye orodha ya wasanii waliotakiwa kutumbuiza katika tamasha moja nchini humo siku chache kabla ya sintofahamu hiyo jambo ambalo Yeezy alifanya sapraizi ya kufika kwenye shoo hiyo.

Aidha, mnamo Februari, Kanye alimwondoa Cudi kwenye orodha ya wasanii aliowashirikisha katika albamu yake ya DONDA 2 kwa sababu tu ni rafiki wa karibu wa Davidson. Cudi alikubali na kumuita Kanye “dinosaur ama mjusi mkubwa,” na kuongeza kuwa, “Wewe sio rafiki yangu.”

Ijumaa iliyopita, taarifa zilianza kusambaa kuwa Pete na Kim wameachana ikiwa ni miezi tisa tu tangu waingie kwenye uhusiano. Ikumbukwe kuwa, Kanye ndiye alikwenda mahakamani kuomba talaka kuomba talaka na Kim licha ya baadaye kubadili maamuzi yake na kutaka talaka hiyo isitolewe lakini Kim amekuwa akisisitiza apewe talaka yake awe huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live