Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West yamkuta tena, avuliwa Shahada ya Heshima

Kanye West Saic Kanye West

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kauli tata za Kanye West 'Ye' anazoendelea kuzitoa kila uchao, zinamgharimu katika maisha yake ya kawaida kwani, amevuliwa Shahada ya heshima aliyopatiwa mwaka 2015 na Shule ya Sanaa ya Chicago, "School of the Art Institute of Chacago"

Taarifa rasmi iliyotolewa na shuke hiyo imeeleza kwamba, imechukua hatua ya kumvua Shahada ya heshima na kufuta shahada hiyo ya Ye. "Kauli zake dhidi ya Weusi, chuki dhidi ya Wayahudi na za uchochezi, haswa zile zinazoelekezwa kwa jamii za Weusi na Wayahudi, ni za kuchukiza na zakulaaniwa".

"Kama Jumuiya, tunajua kwamba kuna maoni tofauti juu ya Shule yetu yanapaswa kuchukuliwa hatua kwa haraka zaidi - hata kama sisi sote tunakubali kwamba tabia yake haiwezi kutetewa". Taarifa hiyo imeandikwa na Mkufunzi wa Shule Bi. Elissa Tenny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live