Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West avunja mkataba na kampuni ya kuuza bidhaa zake

Kanye West@2000x1500 1 Kanye West avunja mkataba na kampuni ya kuuza bidhaa zake

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rappa na mfanyabiashara maarufu Duniani, Kanye West 'YE' anaripotiwa kuwa amefikia maamuzi ya kuvunja mkataba wake na Kampuni Ya GAP iliyokuwa ikihusika na uuzaji pamoja na usambazaji wa bidhaa za #YEEZY.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wall Street Journal, Kanye West ameamua kumtuma mwanasheria wake Nicholas Gravante Jr, kuitaarifu GAP kuwa anasitisha nao mkataba wa ubia katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa zake, ikiwa ni miaka nane imesalia ya mkataba huo.

Fahamu, mkataba wa YE na GAP ulianza rasmi mwaka 2020, ambapo YE alisaini mkataba wa miaka 10 na kampuni hiyo.

Aidha, mapema wiki hii, Ye alizungumza na Bloomberg na kueleza kwamba ni muda sasa wa yeye kufanya biashara peke yake. Alisema hakuna kampuni tena ambayo itasimama katikati yake na watu wake (wateja).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live