Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West ataka aitwe "Ye" aandika barua hii..!

Yeezy Letter Msanii Kanye West (Ye)

Sun, 24 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Marekani Kanye West amezitaka taasisi kubwa katika sekta ya muziki duniani kuheshimu uamuzi wake wa kutumia jina alilolibadilisha kisheria la “Ye” umeripoti mtandao wa TMZ.

Katika barua iliyaondikwa ambayo TMZ imeiona, Mkuu wa Utawala wa Kanye, Milo Yiannopoulos ametoa ujumbe mkali kwa wadau wa muziki, ikiwemo wanaosambaza nyimbo mitandaoni (streamers), wachapishaji, tovuti zinazoandika mashairi ya nyimbo na wengineo, akidai kuwa mwanamuziki huyo lazima aitwe kwa jina la Ye.

Milo amesema Kanye hakufikia uamuzi wa kubadili jina kirahisi, kwa sababu anafahamu ukubwa na thamani ya jina la “Kanye West”, lakini West mwenyewe analiona jina hilo kuwa ni la “kitumwa” na anataka kuachana nalo katika ngazi zote.

Milo ameongeza kusema: “Ye ni mtu mweusi Marekani ambaye anataka haki ya uhuru wake kamili kama mtu yeyote yule.”

Kanye alibadilisha jina lake rasmi kuwa Ye Oktoba 2021. Jaji wa mahakama alisaini mabadiliko ya jina hilo, ambalo lilikuwa jina lake la utani kwa siku nyingi.

Ye sio msanii wa kwanza kubadilisha jina, wengine ni Diddy, Snoop Dogg, Prince, Bow Wow, Kei$ha, na hata 2 Proud kwa Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live