Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West amuomba msamaha Kim Kardashian

Kanye Kim Lao.jpeg Kanye West na Kim Kardashian

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa na bilionea Kanye West amemuomba msamaha kwa “mfadhaiko wowote” aliomsababisha hivi karibuni mke wake wa zamani Kim Kardashian juu ya kulea watoto wao wanne, kupitia mahojiano ya kipindi cha Good Morning America kitachoruka usiku huu.

“Huyu ni mama wa watoto wangu, na ninaomba msamaha kwa changamoto zozote ambazo nimesababishia” alisema West na kuongeza.

“Ninahitaji mtu huyu (Kim) asiwe na msongo wa mawazo na awe na akili timamu na mtulivu iwezekanavyo ili kuweza kuwalea watoto wetu.

“Rapa huyo amesema matatizo yote aliyomsababishia mzazi mwenzake, yanatokana na yeye kuhisi anayimwa haki ya kuwalea watoto wake North, (9), Saint, (6), Chicago, (4), na Psalm, (3).

Katika kionjo cha mahojiano hayo kilichoachiwa mapema leo, Kanye maarufu kama Ye kwa sasa, pia amezungumzia suala la matamanio yake ya kuingia Ikulu ya White House kama Rais wa Marekani, kuwa na “shule ya Injili” chini ya jina la Donda Academy na mwisho kuhusu mpango wake na kampuni ya The Gap.

Nyota huyo wa rap mwenye umri wa miaka 45 na Kim (41), walitalikiana mapema mwaka huu, kabla ya wawili hao kuanza kushambuliana kupitia mahojiano na mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live