Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West amuoa mfanyakazi wake

Kanye Na Mkewe Kanye West amuoa mfanyakazi wake

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa wa muziki kutoka nchini Marekani Kanye West ambaye kwa sasa amebadili jina lake na kujiita Ye amemuoa mfanyakazi wake ambaye ni mbunifu wa kampuni yake ya Yeezy anayeitwa Bianca Censori miezi miwili baada ya talaka yake na Kim Kardashian kukamilika.

Rapa huyo, 45, inasemekana alifanya sherehe ya faragha na Bianca na wawili hao wameonekana wakiwa wamevalia pete za ndoa.

Kwa mara ya kwanza Kanye alipigwa picha akiwa amevaa pete yake wiki iliyopita, huku vyanzo vya habari viliiambia tovuti hiyo kuwa Ye kuonyesha pete hiyo inaashiria kuwaonyesha watu kuwa yupo kwenye ndoa yaani amefanya makusudi.

Licha ya kufanya sherehe ya harusi ndoa hiyo inaelezwa kuwa sio halali kwa sababu wanandoa hao wanaonekana hawajaandikisha cheti cha ndoa, hii ni kwa mujibu wa TMZ.

Haijabainika ni muda gani wawili hao wamefahamiana au wamekuwa wakichumbiana, lakini Bianca alijiunga na kampuni ya Kanye ya Yeezy mnamo Novemba 2020

Chanzo: www.tanzaniaweb.live