Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West amtaani mke wa Obama

Kanye West Amtaani Mke Wa Obama Kanye West amtaani mke wa Obama

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #KanyeWest amefunguka kutamani kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mke wa aliyekuwa Rais nchini humo Baraka Obama, Michelle Obama.

Kupitia mahojiano yake na ‘The Download Podcast’ Kanye aliulizwa swali kuwa ni mwanamke gani mwingine angependa kuwa naye akiachana na mpenzi wake Bianca ndipo akajibu anatamani kuwa na Michelle Obama.

Kanye kwa sasa yupo kwenye ndoa na mwanadada #BiancaCensori ambaye amekuwa akizua gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na aina ya mavazi anayovaa.

Ikumbukwe kuwa wawili hao January mwaka 2023 walifunga ndoa baada ya Kanye kutalikiana na aliyekuwa mke wake na mzazi mwenzie #KimKardashian.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live