Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West, TY Dolla $ign wakwama kuachia albamu

Kanye West, TY Dolla F Kanye West, TY Dolla $ign wakwama kuachia albamu

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Jarida la #Billboard, Rapa Kanye West (YE) na Staa wa R&B, TY Dolla $ign wameshindwa kuachia albamu yao mpya tangu Oktoba 13, 2023 baada ya kukosa Msambazaji kwa kilichodaiwa Wasambazaji wengi wanaikwepa kutokana na kauli tata za YE.

Albamu ya mwisho kutoka kwa Kanye West ni #DONDA2 iliyotoka Februari 23, 2022 kwa utaratibu wa kuuzwa kupitia kifaa cha Muziki cha '#StemPlayer' ambapo alidai ndani ya saa 24 alifanikiwa kuuza nakala 39,000 na kuingiza zaidi ya Tsh. Bilioni 5.57.

Mwaka 2022, Universal Music Group ilitangaza kuwa 'Label' ya #DefJam iliachana na Kanye West pamoja na Label yake ya #GOODMusic tangu mwaka 2021 ikiwa ni baada ya kutoa jumla ya Albamu 10 chini ya #UMG.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live