Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West: Sina ugonjwa akili, nina dalili za usonji

Kanye West Wayahudi Kanye West: Sina ugonjwa akili, nina dalili za usonji

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kanye West ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kumfuata Elon Musk kwenye text messeges na kumwachia ujumbe mzito ambao amemtaka tajiri huyo aufikishe kwa watu.

YE amefunguka hadharani kwamba, hana tatizo la akili ‘Bipolar’ kama ambavyo dunia imeaminishwa bali ana dalili za ugonjwa wa Usonji (Autism) ambao ulitokana na ajali ya gari ambayo aliipata Oktoba 2002.

Usonji ni nini? ni ugonjwa wa neva na wa kiukuaji (developmental disorder) unaoathiri namna mtu anavyoshirikiana na wenzake, anavyozungumza, anavyojifunza, na tabia yake. Miongoni mwa dalili za usonji ni; Watu wenye usonji wana shida katika kufanya mawasiliano na kujichanganya na jamii, kuwa na mapenzi na vitu vichache, na tabia za kujirudia.

Kitaalam zaidi inaelezwa kwamba, Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live