Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanumba angekuwa hai macho yote yangekuwa kwetu - Ben

Kanumba.jpeg Kanumba angekuwa hai macho yote yangekuwa kwetu - Ben

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji Ben wakati akifanya mahojiano na @mwananchiscoop amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya stori ambazo anafikiria kama angekuwepo Kanumba angezifanya vizuri zaidi kuliko zinavyofanywa na waigizaji wengine.

“Kuna stori ambazo huwa nawaza ningekuwa na ile ‘mashine’ yangu Kanumba basi kila mtu angeacha kuangalia kwingine angetutazama sisi tu, lakini ndiyo hivyo hayupo tena,” amesema

Hata hivyo mwigizaji huyu ameenda mbali zaidi na kuieleza mwananchi scoop kuwa enzi hizo walibahatika kucheza filamu na watu wa nje ya nchi, wamejifunza mambo makubwa na ndiyo maana kwa upande wake hapati tabu kwani hakuna kitu kigeni na ndiyo maana akipewa uhusika wowote anautendea haki.

“Sisi tuliobahatika kucheza na wasanii kutoka nchi nyingine tumebahatika kuwa na madini makubwa na ndiyo maana mimi ukiniweka popote nanyoosha kwa sababu hata robo hatujawafikia wasanii wa nje,” amesema Ben .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live