Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni za kusambaza filamu zaanguka, JB aomba msaada wa serikali(Video)

7415 JB TZW

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii mkongwe wa filamu nchini Tanzania, Jacob Stephan aka JB amefunguka kuiomba serikali kuingia kati na kutatua changamoto ambayo inazikuta kampuni nyingi za kusambaza filamu nchini Tanzania.



Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, JB amesema kampuni ambayo kwa sasa inajiendesha kwa shida ni Steps pekee kwani kampuni nyingi ikiwemo yake ya Barazani na nyingine hali yake ni mbaya.

“Kusema kweli hali sio nzuri kabisa serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kuweza kuinusuru hii hali, Proin imekufa, Barazani ndio hivyo, yaani mambo yamekuwa mabaya sana kila kukicha, mimi binafsi naomba serikali ifanye uchunguzi iangalie nini kinasababisha kampuni nyingi kushindwa kujiendesha,” alisema JB.

Aliongeza, “Tatizo sio soko, watanzania wanataka sana filamu zetu, tatizo ni usambazaji, namna ambavyo unaweza kupenyeza filamu zetu kila kona, na kwanini kampuni za wazawa ambazo zinajaribu kufanya hii biashara zinashindwa na baadaye zinafungwa,”

BJ amesema hao Steps ambao wanaonekana kuwa kama wakombozi na wao wameanza kuzidiwa nguvu kutokana na mazingira ya soko kuwa mabaya kila kukicha.

Loading...
Chanzo: bongo5.com