Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni iliyomsimamia Diamond kununua ndege na helkopta yafunguka

Diamond Ndege Tenaaaa Kampuni iliyomsimamia Diamond kununua ndege na helkopta yafunguka

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku chache baada ya Supastaa wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya WCB, Diamond Platnumz kutangaza kukununua ndege binafsi, kampuni ya V III Aviation ambao wamemsaidia msanii huyo kufanya manunuzi ya ndege hiyo wamefunguka mengi.

Yusuph Kazi ambaye ni CEO wa kampuni hiyo amesema kuwa ndege ya Diamond ni kubwa na ina uwezo wa kusafiri masafa marefu bila kutua huku akibainisha kuwa ndege hiyo ina injini mbili na ina uwezo mkubwa.

Kazi amebainisha kuwa si ndege tu, bali Diamond amenunua pia helkopta ambapo atazitumia kwa kazi zake za Sanaa na hata katika biashara ama dharura za matibabu kwa kuwa zina mfumo huo.

“Diamond kununua helkopta sio ishu kwa sababu ni msanii mkubwa, uwezo wa kununua anao, niwathibitishie tu kwamba ni kweli Diamond amenunua ndege (private jet) na helkopta ili kumsaidia katika mambo yake na sisi tumemsaidia sana katika kununua ndege hizo. Mpaka sasa watalaam wetu wapo kule wakihakikisha kila kitu kiko sawa ili ziweze kufika nchini.

“Siwezi kusema amenunua kwa shilingi ngapi kwa sababu mimi sio msemaji wake, lakini unaweza kupata chopa kwa dola milioni 3 (zaidi ya Tsh bilioni 6.9) au dola milioni hata dola milioni 2 unaweza kupata, inategemeana na chombo unachokitaka na matumizi yako.

“Wasafi ndio watatupa utaratibu ni lini itafika baada kukamilisha kwa taratibu zote za kiserikali, basi mtaona kitu kimeingia nchini. Tufahamu kuwa Diamond amefanya kitu kikubwa sana Afrika Mashariki hata sisi hatuna hiyo helkopta aliyochukua, itasaidia hata kuitangaza Tanzania.

“Helkopta aliyonunua Diamond inaweza kuruka usiku na mchana, ni twin engine (ina injini mbili), anaweza kutumia anavyoweza kulingana na taratibu za Mamlaka ya Anga, inabeba mafuta mengi anaweza kuruka Dar mpaka Mwanza moja kwa moja bila kutua. Uwezo wa chombo ni mkubwa sana.

“Taratibu za kununua ndege na helkopta ni zilezile, kasoro ni kwamba helkopta inaweza kuwa na viwanja vingine vidogovidogo. Juzi alitoka Afrika Kusini akatua Kenya kisha akapande chopa, ile kuruka na jet halafu anapanda helkopta, alikuwa anatuma salam kwa watu wake kwamba kuna kitu kinakuja.

“Kununua jet na helkopta itamsaidia kwamba anaweza kufika sehemu anatakwenda hakuna uwanja wa ndege, kwa hiyo akishuka kwenye ndege anaweza kupanda helkopta ikampeleka anapotaka kufika akafanya mambo yake akamaliza akarudi.

“Mtu binafsi kununua ndege sio tatizo, Diamond akuwa na ndege kuna faida nyingi kama Taifa. Anaweza akaitumia katika shughuli zake, lakini pia anaweza kuikodisha watu wanataka kwenda kwenye mikutano nje ya mkoa ama nje ya nchi kwa haraka, pia inaweza kusaidia pengine kuna mgonjwa anatakiwa kuwahishwa Afrika Kusini ama India kwa matibabu,” amesema Kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live