Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamishna wa Madawa aonya wasanii kutunga nyimbo za kuhamasisha bangi

Kamisha Madawa Kamishna wa Madawa aonya wasanii kutunga nyimbo za kuhamasisha bangi

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya amewaonya Wasanii wa Tanzania wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa Wasanii hao.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo amesema;

“Kuna Wasanii wanahamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi, kama kuna Wasaniii ambao wanadhani badala ya kutunga nyimbo za kuhamasisha Jamii wao wanatunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya, sheria yetu inasema hao tutawachukulia hatua.

“Kama kuna Msanii anadhani anaweza kupata umaarufu kwa kupitia nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya hatutomuacha hata mara moja, sheria itachukua mkondo na ipo siku nitawaita Waandishi wa habari ili muone kitu gani tumekifanya kwa Wasanii wanaotaka kupata umaarufu kwa kutumia dawa za kulevya.

“Mbona mashairi yapo ya aina nyingi unashindwaje kutunga mashairi ya vitu vyote, si wahamasishe hata kilimo bora au biashara, kwani lazima wahamasishe mambo ya bangi? hatutoruhusu Mtanzania yoyote afanye uhamasishaji wa matumizi ya dawa za kulevya," asema Kamishna Gerald Kusaya.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya msanii wa Bongo Fleva, Harmonize kuachia wimbo wa Weed Language.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live