Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kamera za ndani marufuku AirBNB

Airbnbbb Kamera za ndani marufuku AirBNB

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya AirBNB inayowezesha Watu mbalimbali duniani (ikiwemo Tanzania ) kukodisha makazi ya muda mfupi kwa njia ya mtandao, imepiga marufuku Wamiliki kuweka camera za usalama ndani ya nyumba kutokana na wasiwasi wa ukiukwaji wa sheria za faragha.

Kampuni hii iliyoanzishwa mwaka 2008 ikiwa na Makao yake Makuu San Francisco, California nchini Marekani, hadi sasa imekua ikiruhusu matumizi ya camera za usalama katika maeneo ya kawaida kama vile sebuleni (sitting room) ilimradi zisiwe zimefichwa na ziweze kuonekana kwa urahisi na Wageni.

“Mabadiliko haya yamefanywa kwa kushauriana na Wageni wetu, wenye Nyumba na Wataalamu wetu wa masuala ya faragha na tutaendelea kuyapokea maoni zaidi ili kusaidia kuhakikisha sera zetu zinafanya kazi kwa jumuiya yetu ya kimataifa” - amesema Juniper Downs, Mkuu wa sera na ushirikiano wa Airbnb.

Hatua hiyo imekuja baada ya miaka mingi ya ripoti za mara kwa mara za Watumiaji wa Airbnb kugundua camera zilizofichwa kwenye makazi yao ambapo Airbnb imekua ikiwajibu kwa kusema itafanya uchunguzi.

Kampuni ya ‘Airbnb’ pia ilisema wenye nyumba bado wataruhusiwa kuweka camera za usalama karibia na mlango ili kushughulikia masuala ya kiusalama lakini wenye nyumba watahitajika kuiambia AirBNB kuhusu uwepo wa camera hizo pamoja na idadi ya camera zilizowekwa nje ya nyumba kabla ya kukubali maombi ya Wateja watakaotaka kukaa katika nyumba hizo.

Camera zilizowekwa nje pia hazipaswi kutumika kama njia za kufuatilia yanayoendelea ndani ya nyumba au vyumba, taarifa ya AirBNB ilisisitiza na kusema sera hiyo iliyorekebishwa itaanza kutumika kuanzia April 30 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live