Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamera na kalamu ya udaku vilivyomulika na kuwaanika mastaa wa Bongo

Kanumba Wema Kamera na kalamu ya udaku vilivyomulika na kuwaanika mastaa wa Bongo

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama Kuna nyakati ambazo Magazeti ya Udaku yaliuza sana, ni nyakati ambazo Watanzania hatuna uelewa wowote kuhusu Instagram Facebook Twitter na WhatsApp, ni nyakati ambazo hata waliomiliki simu walikuwa ni wachache sana.

Hapa ndipo Camera za Mapaparazi zilipofanya kazi yake, kwa kumulika maisha ya mahusiano ya Mastaa wetu, na kisha kutuhabarisha kupitia Magazeti yao ya Udaku.

Picha linaanza ndani ya giza zito Camera ya paparazi inammulika Jumanne Kihangala, wengi tulimtambua kwa jina la Mr Chuz, huyu alikuwa mkurugenzi wa Fukuto Arts group, kundi ambalo lilibamba sana na Tamthilia ya Ua Jekundu, na baadaye Jumba la Dhahabu, Kalamu ya paparazi, inamtaja muigizaji, Jacqueline Steven Pentzel kunasana kwenye penzi la Mr Chuz, penzi lake na Chuz lilibamba sana, wawili hawa walionekana kupendana sana.

Kiasi cha kupelekea Jacqueline ajiite Jacky wa Chuz, penzi lilifikia hatua ya kutangaza ndoa.

Wadau wa udaku tukawa tunasubiri muendelezo wa hili penzi. Huku Tukiwa na matarajio ya kuona wawili hao wanafunga ndoa.... Aaah Salamaleko walah!!! Kwani ndoa ilifungwa sasa?

Sijui ni mdudu gani kisirani aliingia katikati ya utamu wa penzi la wawili hawa, wakabwagana. Na kila mmoja kushika utaratibu wake.

Huku na kule Camera inammulika tena Mr Chuz, safari hii tunahabarishwa kuwa bosi huyo wa Jumba la dhahabu, yupo katika uhusiano wa kimapenzi na dada mmoja wa kazi wa nyumba ya jirani yake, ingawa hili Mr Chuz alilikataa kuwa hayupo katika uhusiano na huyo Msichana.

Mapaparazi na Camera zao wakaingia tena kazini, kutaka kujua kama hayupo katika uhusiano na dada huyo, yupo na Mwanamke gani. Wakaenda kumuibua Leila Ismaili, kwa kizazi cha miaka ya elfu mbili, hili jina la Leila Ismail ni geni kwao.

Naomba niwaambie tu Leila Ismail ni msanii wa maigizo, aliwika sana enzi hizo na kundi la Nyota Ensemble Mambo Hayoí, Mr Chuz na Leila Ismail katika uhusiano wao, waliweza kupata mtoto mmoja kabla ya kumwagana.

Mr Chuz alikuwa ni lover boy mtupu, hakuna Mwanamke ambaye alimchekea halafu akamuacha salama. Mshikaji aliwahi kuripotiwa kutoka na muigizaji ambaye pia ana kipaji cha kuimba, Joan Matovolwa, ingawa hili walitaka kufanya siri, lakini ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi kati yake na staa anayetambulika kwa uhusika wa kijini, Miriam Jolwa Jini Kabula uliwekwa kila kitu kweupe.

Habari zilisema kuwa Chuz alianza kutoka na Joan kabla ya kuhamishia majeshi kwa Kabula, na ishu nzima ilipovuja, ikawa ugomvi usio na mwamuzi kati ya msanii huyo na Kabula aliye mzazi mwenza wa mkurugenzi huyo wa Fukuto Arts group, Joan ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Flava, marehemu Steve 2K aliyefariki dunia mwaka 2004 kwa kuchomwa kisu na mtayarishaji wa muziki Castro, ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye Studio ya Baucha, Kumbuka kuwa Joan, Jini Kabula na Jacqueline Steven Pentzel, hawa wote walikuwa katika kundi la maigizo la Fukuto, ambalo mmoja wa kiongozi wake ni Mr Chuz, kifupi ni kwamba jamaa alikuwa anawakula wasani wake, ndiyo maana nasema jamaa alikuwa Lover boy mtupu.

Baada ya ugomvi huo wa Kabula na Chuz. Kalamu ya mwandishi iliandika kuwa, Jini Kabula kwa sasa yupo kwa Mfalme wa Takae, Nice Lucas Mkenda Mr Nuce, ambaye ni mzazi mwenzake na mnenguaji marehemu Diana Aston Villa, ambaye enzi za uhai wake naye aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na mchekeshaji maarufu nchini, Steven Mangere Nyerere.

Kwa upande wa Joan yeye baada ya hapo, akahusishwa kutoka kimapenzi na Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El-Saadat ambaye ni mjane wa mnenguaji mwenye jina kubwa Bongo, marehemu Rukia Bruno. Marehemu Rukia Bruno aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na Marehemu Kanumba, na baada ya kumwagana na Rukia, Kanumba alijiweka kwa Maadam Wema Sepetu, na akaganda hapo mpaka kuibuka kashikashí za kugombana na kufikishana mahakamani.

Kanumba pia amewahi kuripotiwa kutoka kimahaba na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed ambaye alikuwa mchumba wa mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Masoud Kipanya.

Wadaku tunajua kuwa, ustaa wa Wema ulianza kuandikwa, kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa Bongo Flava, Khaleed Salum Mohamed TID, ambaye aliwahi kuripotiwa kutoka na mrembo wa kizungu.

TID pia, aliwahi kuandikwa kuhusu kumpa ujauzito binamu yake ambaye walikuwa wanaishi nyumba moja, nyumbani kwao, Kinondoni Dar, lakini mwanamuziki huyo aliikana mimba hiyo.

Camera ya paparazi inammulika Dogo aliyekuja kwa kasi sana katika ulingo wa Bongo Flava, Ni Heri Samir ukipenda muite Mr Blue, Kijana anaungwa katika Listi ya mwandishi, baada ya kuwa kati ya wanaume wa kwanza kwanza kuandikwa, wakihusishwa na penzi la Wema Sepetu.

Ustaa wa Wema Sepetu ulianza na Skëndo nyingi sana, magazeti ya udaku yaliuza sana habari za Miss Tanzania huyu wa mwaka 2006.

Kwa nyakati tofauti Wema aliandikwa kutoka kimapenzi na mheshimiwa mmoja nchini jina kaponi, na pia aliwahi kuhusishwa kutoka na Mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe, na waliishi kama mke na mume, na kujitangaza kwamba wao ni wanandoa halali kabla ya kuachana kwa mbwembwe.

Wema alizidi kushikilia vichwa vya habari, baada ya kuripotiwa kutoka kimapenzi na Brazamenií wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta International, Charles Gabriel Mbwana, jina la kisanii Chalz Baba, pamoja na Mkurugenzi wa Hartmann Production, Hartmann Osmund Mbilinyi. Hartmann pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Miss Mwanza 2006, Aunt Ezekiel na dada anayekwenda kwa jina la Linah.

Watu wa udaku tukashangaa kwakuwa Hartmann alikuwa ana mke wake anayeishi Uingereza. Kwa upande wa Aunt Ezekiel pia amewahi kuhusika kimapenzi na Mtanzania asiyejali thamani ya fedha katika matumizi, aitwae Jack Pemba, ambaye baada ya kuachana na Aunt Ezekiel, alijirusha na mrembo mmoja wa Kibongo, wakati huo huo akiwa na mke wake mzungu nchini Uingereza.

Kwa upande wa Chalz Baba, siyo stori kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kimwana manywele namba mbili 2007, Husna Sajenti, wakati huo huo akiwa amekorofishana na mrembo aliyekuwa akiishi naye kinyumba, anayekwenda kwa jina la Mariam.

Baada ya kubaini alikuwa yupo kimapenzi na mzungu. Chalz pia kabla ya kuwa na Mariam aliwahi kuwa na uhusiano wa kudumu na mrembo anayekwenda kwa jina la Sada, wakati huo huo mwanamuziki huyo akiwa ni mzazi mwenzake Mama Jack.

Huo ni udaku ambao tuliufaidi enzi hizo kupitia Magazeti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live