Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati Teule Tuzo za Tanzania (TMA)

Kamati TMA Kamati Teule Tuzo za TMA

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uteuzi umefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Damas Ndumbaro na sasa hii ndio Kamati itayohusika kuratibu Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kwa mwaka 2023-2024.

Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kupitia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Kedmon Mapana limemwaga baraka zake leo kwa kamati hiyo mpya ambayo BASATA imesema imeshaanza kazi.

“Kutana na Timu mpya yenye weledi na ubobevu ya Tuzo za Muziki za Tanzania 2023, Timu hii ya nguvu iko tayari kuinua Tuzo za Muziki Tanzania kwa viwango vipya, kwa ujuzi wao usio na kifani na mtazamo wao wa kipekee, watarekebisha tasnia ya muziki na kukuletea TMA ambayo haijawahi tokea, jiandae kwa mafanikio ya kuvunja rekodi” amesema Dr. Mapana.

Kamati hii inaongozwa na Mwenyekiti David Minja, Makamu Mwenyekiti Christine Mosha, Katibu Mrisho M.Mrisho na Wajumbe ambao ni Producer P Funk, Chris Torline na Natasha Stambuli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live