Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama unaimba amapiano, wewe ni feki - Master Jay

Ama Masta Jay Master Jay

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Producer nguli wa muziki wa Bongo, Joachim Marunda Kimaryo maarufu kama Master Jay amesema kuwa yeye hajazuia wala kuwaponda wasanii wanaoimba muziki wa Amapiano bali amewashauri wasiimbe Amapiano kama ya Afrika Kusni kwani si utambulisho wa muziki wa Bongo.

Master Jay amewataka wasanii wa sasa kama wanataka kuimba amapiano basi wachanganya iwe Amapiano ya Kisingeli ama ya Kibongo Fleva ili kuleta utofauti na ile inayoimbwa na Wasauzi kwani inaupoteza muziki wa Tanzania kwenye ushindani wa Kimataifa.

Kauli ya mkongwe huyo wa muziki inakuja wakati kukiwa na wimbi la wasanii wengi wa Bongo kuimba Amapiano, muziki ambao si identity ya muziki wa Bongo Fleva ama aina yoyote ya muziki kutoka Tanzania.

"Mimi sijasema watu wasifanye Amapiano, ninachosema 'don't copy and paste', huu sio ubunifu, mtu yeyote anaweza kukopi. Chukua Amapiano changanya na Singeli.

"Ni vitu vidogo vidogo, hakuna mtu kasema mtu asifanye Amapiano lakini fanya Amapiano kama yenyewe lakini fanya vilevile Amapiano themes na Singeli au Amapiano na Bongo Fleva ili uwe na sound ambayo ni unique kwako wewe.

"Huwezo kusema unaimba international unaimba Amapiano halafu unatoka Tanzania bro, ile sio identity yetu na huwezi, as long as umesema wewe unaimba Amapiano wewe ni feki," amesema Master Jay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live