Meneja maafuru wa wasanii kutoka WCB Sallam Sk ametoa somo la njia mbadala ambayo baadhi ya wasanii wanapaswa kuifuata kuliko kuendelea kufanya muziki kwa kipindi kirefu bila mafanikio yeyote, huku akisisitiza kuwa sio kila msanii ananafasi ya kufanikiwa sawa na wengine na kwamba wasanii wa muziki ambao wamehangaika kwa muda mrefu bila kufanikiwa wanapaswa kubadilisha mtazamo ikiwezekana kuugeukia upande wa usimamizi wa kazi za wasanii badala.
Sallam ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuyasema hayo huku akisisitiza kuwa ni muhimu kusoma alama za nyakati, na kwamba wakati mwingine mafanikio ya kimuziki huokea kwa bahati na si, ujanja wa mtu binafsi.
“Muziki ulivyo, unaweza kuwa na talent lakini ukakosa kitu kinaitwa “BAHATI” ushauri wangu kama umefanya muziki kwa muda mwingi na haujakulipa geukia upande wa pili wa Management sababu kuna uhaba wa managers wenye upeo na muziki kwenye industry yetu. Happy New Year,” ameandika Sallam.
Kauli ya meneja huyo imeonekana kupokelewa vizuri na idadi kuwa ya wafuasi wake mtandaoni, ambao kwa kiasi kikubwa wameshiriki maoni yao kama sehemu ya kuunga mkono wazo hilo.