Watu wengi wamezoea kuona mwanaume anamuoa mtu ambaye si damu yake yaani waliozaliwa na baba na mama mmoja, hii ni kutokana na maandiko ya vitabu vya dini na jamii nyingi huamini katika hilo.
Lakini imekuwa tofauti sana na kijana mmoja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paulen Ziarirwa mwenye umri wa miaka 28 ambaye amemuoa dada yake wa damu aitwaye, Dorica Ziarirwa mwenye umri wa miaka 26.
Wanandoa hawa wamezaliwa kwenye familia moja kutoka kijiji cha Bunia ambacho kilitokea mgogoro wa kikabila na kusababisha watu kuuawa na wengine kukimbia makazi yao.
Paulen na Dorica Ziarirwa wakakimbilia sehemu ambayo inaitwa Miti na wasamaria wema wa eneo hilo wakawalea na kuishi nao na baadaye Paulen akaamua kurudi kijijini kwao Bunia kwa ajili ya kwenda kuwatafuta wazazi wao lakini hakifanikiwa.
Baada ya hapo akarudi kijijini kwao na walikaa hapo kwa muda mrefu hadi ikafikia wakati ambao anahitaji kujitegemea na ndipo akawaza kuishi na dada yake Dorica, mawazo hayo yakampelekea Paulen kutaka kumuoa dada yake, akaamua kumwambia dada yake kuwa anampenda na anataka kumuoa ili waanzishe familia.
Dorica akamwambia kaka yake Paulen kuwa inabidi wahame eneo hilo kwa sababu wanajua wao ni ndugu hivyo jamii itawachukulia tofauti, ndipo wakaamua kuhama eneo hilo na kwenda eneo linaloitwa Kashegema kisha kuanzisha familia yao.
Wanandoa hawa wakapata watoto nne na mtoto wao wa kwanza anaumri wa miaka 8 na tayari wamefikisha miaka 10 ya ndoa yao.
Paulen amesema dada siyo mama hivyo alichokifanya ni sahihi na wala hajutii kufunga ndoa na dada yake na kwamba wanajaribu kila namna ili watoto wao wasijue ukweli kuhusu wao kwa sababu ni ngumu sana kuwaambia na hapo baadaye wakiwa wakubwa watatafuta njia ya nzuri ya kuwaambia ukweli.
Dorica amesema kuishi na kaka yake ni vizuri sana kwa sababu kila mmoja anamfahamu vizuri mwenzake hivyo hawezi kumdanganya na hakuna anayemsaliti mwenzake.
Naye, jirani yao Rose Mary Feza amesema kwamba alisikia fununu kuhusu wanandoa hawa kama ni ndugu lakini hana uhakika kwa sababu hawajawahi kuweka wazi kuhusu mahusiano yao.
Ameongeza kuwa kuna siku mwanakijiji mmoja aliwafuata wanandoa hao na kuwaambia kuwa wao ni ndugu wa damu, Dorica alikasirika na kuwapeleka kwa uongozi wa kijiji, huku wengine wakiamini kuwa wawili hawa walitoka familia mbili tofauti na ndipo wakakutana pamoja na kupendana.
Pauline mwenye amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kukiri kuwa wao ni ndugu wa damu na endapo wazazi wao watagundua hilo hawataweza kuachana, kwa sababu tayari wana watoto wa nne.