Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala na mwanae wawapeleka Rayvanny, Harmonize studio

Harmo Pic Data Kajala na mwanae wawapeleka Rayvanny, Harmonize studio

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rayvanny, Harmonize wachapana studio. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wawili hao kuachia nyimbo zao kwa siku moja. Nyimbo hizo zilizoachiwa jana Jumatatu Aprili 12,2021 ni ‘Nyamaza’ ulioimbwa na Rayvanny na ule wa ‘Vibaya’ ulioimbwa na Harmonize. Wa kwanza kuachia wimbo ni Harmonize aliouachia saa moja usiku katika akaunti yake ya YouTube huku akiweka kipande cha picha ya gazeti lilioandikwa Harmonize vibaya na jina la aliyetayarisha wimbo huo ambaye ni Boy Beat. Pia katika picha hiyo kulia kuna picha yake akiwa na Kajala wakiwa wameshikana mkono ikiwa nusu kuanzia kifuani kushika chini. Wakati kwa Harmonize ikiwa hivyo, Rayvanny yeye hajaweka mambo mengi katika cover ya wimbo wake zaidi ya kuweka maandishi yanayosomeka ‘Nyamaza’. Ukisikiliza kwa makini nyimbo zote mbili ni wazi zinazungumzia yanayoendelea mitandaoni kuhusu kuvunjika kwa penzi kati ya Harmonize na Kajala na kuelezea kiini cha mzozo huo kinachohusishwa na kumtaka mtoto wa Kajala kimapenzi ambaye anaelezwa pia yupo katika mahusiano na Rayvanny.

Rayvanny, Harmonize wachapana studio. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wawili hao kuachia nyimbo zao kwa siku moja. Nyimbo hizo zilizoachiwa jana Jumatatu Aprili 12,2021 ni ‘Nyamaza’ ulioimbwa na Rayvanny na ule wa ‘Vibaya’ ulioimbwa na Harmonize. Wa kwanza kuachia wimbo ni Harmonize aliouachia saa moja usiku katika akaunti yake ya YouTube huku akiweka kipande cha picha ya gazeti lilioandikwa Harmonize vibaya na jina la aliyetayarisha wimbo huo ambaye ni Boy Beat. Pia katika picha hiyo kulia kuna picha yake akiwa na Kajala wakiwa wameshikana mkono ikiwa nusu kuanzia kifuani kushika chini. Wakati kwa Harmonize ikiwa hivyo, Rayvanny yeye hajaweka mambo mengi katika cover ya wimbo wake zaidi ya kuweka maandishi yanayosomeka ‘Nyamaza’. Ukisikiliza kwa makini nyimbo zote mbili ni wazi zinazungumzia yanayoendelea mitandaoni kuhusu kuvunjika kwa penzi kati ya Harmonize na Kajala na kuelezea kiini cha mzozo huo kinachohusishwa na kumtaka mtoto wa Kajala kimapenzi ambaye anaelezwa pia yupo katika mahusiano na Rayvanny. Katika wimbo huo wa vibaya, Harmonize anasikika akilalama picha zake za aibu  mpenzi wake huyo asijaribu kuzirusha mitandaoni kwa kuwa hamkomoi. Picha ambazo pia Rayvanny alizizungumzia katika waraka alioundanika siku moja iliyopita kwa kumtuhumu msanii huyo kwa kitendo alichofanya cha kumtumia picha chafu binti huyo. Pia katika wimbo huo msanii huyo ameeleza namna alivyokubali kuachana na aliyekuwa mkewe Sarah na kumsihi amtunze mtoto wake kwani anahisi kuna kamchezo na watu wenye majungu. Wakati katika wimbo wa Rayvany wa Nyamaza, yeye kagusia baadhi ya maneno yanayohusishwa kuwa amemlenga moja kwa moja Harmonize, kwani humo ndani kuna maneno kama Tembo, kaka wa Mtwara. Mfano katika moja ya beti inasema ukakesha hukutaka kula ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara. Pia kuna ubeti Rayvanny kaimba ubinadamu umekuwa majanga,Tembo amefungwa kwa banda anataka kula kuku pia na vifaranga. Ikumbukwe Aprili mwaka huu baada ya Rayvanny kuweka picha chafu zikimuonyesha akiwa na Paula ambaye ni mtoto wa Kajala, Harmonize aliandika waraka mzito wa kumlaumu msanii huyo kwa kitendo alichokifanya huku akitaka vyombo vya dola kumchukulia hatua kwa kumdhalilisha Paula na kumtaka Rayvany kuomba msamaha. Hivyo ni kama Rayvanny naye katika wimbo huo kumuuliza boss huyo wa lebo ya Konde Gang kafanya nini na yeye licha ya ushauri aliompatia wakati sakata lake na Paula lilivyokuwa moto hadi kufikishwa Polisi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz