Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala kumbadili dini Harmonize? Ampeleka kanisani

Kajala Na Harmonizeee Kajala kumbadili dini Harmonize? Ampeleka kanisani

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize huwenda amebadili au kubadili dini hapo baadaye kutokana na kuvutwa kimahaba na mpenzi wake Kajala Masanja.

Gumzo la picha zinazomuonesha Harmonize akiwa kanisani na Kajala zimeibuka jana wakati staa huyo alipokuwa mkoani Lindi katika Uwanja wa Ruangwa mkoani Lindi.

Harmonize ni Muislamu kindakindaki tangu utotoni na alizaliwa katika familia ya Kiislamu huku mpenzi wake Kajala akiwa ni wa dini ya Kikristo.

Suala la dini bila shaka huwa kigezo katika ndoa na baada ya wawili hao kuvishana pete za uchumba, maswali yalikuwa mengi kuhusu mustakabali wa dini ya kila mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live