Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala avunja ukimya picha utupu inayosambaa

115740812 125251099247381 5056184192045465913 N 480x400.jpeg Kajala avunja ukimya picha utupu inayosambaa

Mon, 7 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Staa wa Filamu Kajala Masanja amevunja ukimya kwa kusema hajafikia hatua ya kukaa mikao isiyokuwa na maadili kama inavyosemekana kwenye mitandaoni kuwa picha ya utupu ni yake na Mwanae.

Kajala amekanusha hilo kupitia page yake ya Instagram ambapo ametoa taarifa ndefu inayoelezea tukio hilo kwa kuandika kuwa,

“Kumekuwa na picha ikisambaa ikiwaonesha wanawake wawili wakiwa watupu kwenye mkao usiofaa na wanawake hao wameonekana wakitofautiana umri, picha hiyo ikaeditiwa na kuwekwa kichwa changu ama kinachofanana na changu huku watu wakisambaza kwa kusema ni mimi na mwanangu“.

“Hata kama nina ushenzi wa namna gani sijafikia na wala sitafikia huko hiyo ni laana iliyopitiliza sijui waliofanya hivyo wana malengo gani na mimi, sijawahi na sitawahi kupiga picha ya namna hiyo na binti niliyembeba tumboni miezi 9 na kumzaa kwa uchungu“.

MAJONZI, VILIO VYATAWALA KANISANI KWA TB JOSHUA, UMATI WAJITOKEZA

Chanzo: millardayo.com