Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala amsapraizi Paula kwa ndinga mpya

Therealpaulahkajala 269951508 316626103718425 7117840150700802806 N Kajala na Paula

Sun, 8 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kajala na mtoto wake Paula bado wanaendelea kuzikama headline, safari hii ni zawadi ya gari kutoka kwa mama.

Siku chache baada ya kuachana na Harmonize Frida Kajala amehamishia uzito wa penzi lake kwa mtoto wake Paula Kajala.

Frida amemshangaza (Suprise) binti yake kwa kumnunulia zawadi ya gari aina ya Toyota Crown mpya.

Paula akiwa mwenye shauku, hakuweza kuficha furaha yake baada ya kupokea zawadi hiyo maalum kutoka kwa mama yake mzazi, ambapo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameweka wazi kuwa alitarajia kupata zawadi lakini si nzuri na kubwa kama aliyopatiwa na mama yake.

“Nilijua 2023 itakuwa nzuri lakini sikujua inaweza kuwa nzuri hivi. Kuna akina mama na kuna mama yangu, siwezi kufikiria maisha yangu bila wewe, Asante Kajala Fridah,” Paula aliandika.

Mwaka 2022 ilishuhudiwa maisha ya mapenzi yaliyokuwa dhahiri mitandaoni kati ya Frida Kajala na binti yake yakiishia njiani bila mafanikio baada ya wote wawili kuachana na wapenzi wao wa zamani.

Paula aliachana na aliyekuwa mpenzi wake mwimbaji Rayvanny mnamo Septemba 2022, ambapo Rayvanny ambaye jina lake halisi ni Raymond Shaban Mwakyusa alithibitisha kuachana kwao wakati wa onyesho wa onyesho lake huko Sumbawanga kuwa ameachana na Paula.

Nyota huyo ambaye ni Rais wa Next Level Music aliwaambia mashabiki wake kwamba hayuko kwenye uhusiano, na kuwataka mashabiki wake kamwe wasiruhusu mapenzi kuwachanganya.

“Usiruhusu mapenzi yakuchanganye, usifananishe mapenzi na chakula, nilihitaji amani ya moyo wangu na kukatisha uhusiano wangu na Paula,” Rayvanny alisema.

Frida Kajala kwa upande wake alimalizana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye naye ni Rais wa Konde Music Worldwide Harmonize katika mazingira yasiyoeleweka kutokana na kuwa sababu za wawili hao kutengana kutowekwa hadharani.

Licha ya fununu za chini chini zikidai kuwa chanzo cha wawili hao kutengana ni usaliti uliokuwa ukifanywa na Kajala ambaye alikuwa akishutumiwa kutoka kimapenzi na kigogo, jambo ambalo punde baada ya kumfikia Harmonize, ghafla nuru ya penzi lao ikaanza kufifia na hatimaye kuachana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live