Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala ampotezea Rayvanny

Kajala Pic Data Kajala ampotezea Rayvanny

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

INA maana ndio Kajala Masanja ampotezea Rayvanny.

Hivyo ndivyo unaweza kujiuliza au kusema baada ya msanii huyo kutoka WCB kuomba msamaha na kutojibiwa hadi sasa na mrembo huyo kutoka kiwanda cha Bongomovie.

Wawili hao walijikuta katika wakati mgumu Februari 14 mwaka huu hadi kufikia hatua ya kufikishana Polisi.

Hii ni baada ya Rayvanny ambaye jina lake halisi ni Raymond Mwakyusa, kupost video ya Paula ambaye ni mtoto wa Kajala kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ikiwaonyesha wapo katika mahaba mazito.

Baada ya ukimya wa takribani wiki mbili tangu kutokea kwa tukio hilo Rayavanny hakuwahi kuzungumza lolote kuhusu sakata hilo mpaka Machi 5 alipoandika kwenye ukurasa wake kumuomba msamaha Kajala.

Andiko hilo lilisomeka hivi; “Duniani wakati mwingine kuna vitu tunavifanya ambavyo pengine kwa macho yetu ya ujana tunaona ni sahihi lakini tunasahau upande mwingine wa pili ambao ni wazazi wanaoumia kwa namna moja au nyingine.

Related BABU TALE APIGA MARUFUKU MUZIKI KUPIGWA KWAKE“Nichukue nafasi hii kumuomba radhi dada yangu Kajala Masanja na kuwaomba radhi wazazi na yeyote ambaye nilimkwaza kwa kuposti video ambayo inawezekana imetafsiriwa vibaya …kwa sababu sisi ni binadamu na kamwe hatuwezi kukamilika” alisema Rayvanny.

Pamoja na hatua alizochukua Rayvanny ni kama Kajala ameamua kumchunia na kuamua kuponda raha na mpenzi wake Harmonize, moja ya ‘couple’ ambayo imekuwa gumzo kwa sasa.

Hivi karibuni alipoulizwa na Mwanaspoti ni namna gani anachukulia ukimya huo, Rayvanny alisema asingependa kuliongelea jambo hilo kwa kuwa bado lipo polisi na mazungumzo yanaendelea.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz