Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala ammwagia sifa Harmonize: Nina mume bora zaidi duniani!

Harmonize Na Kajalaaaa Kajala na Harmonize

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu wa Bongo Movies, Frida Kajala Masanja alishindwa kuizuia furaha yake baada ya mchumba wake Harmonize kumzawadia mkufu wa thamani.

Konde Boy alimkabidhi mpenzi wake zawadi hiyo mmoja mnamo siku ya kuadhimisha uchumba wao. Wachumba hao waliadhimisha miezi miwili ya uchumba wao jana Agosti 25. Ili kuonyesha upendo wake kwa Kajala, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alim-surprise mchumba wake wake kwa cheni hiyo ya thamani.

"Niko na mume bora zaidi duniani @harmonize_tz. Shukran hommie," Kajala alieleza furaha yake kupitia ukurasa wake wa Insatagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na video iliyoonyesha mkufu huo wa rangi ya dhahabu ambao alikabidhiwa na mchumba wake. Kwenye ukurasa wake, Harmonize alionyesha picha iliyodokeza walikuwa na mipango maalum ya kuadhimisha siku ya uchumba wao

"Kama vile jana usiku. Nakupenda sana bro @Kajalafrida," Aliandika Harmonize.

Mnamo Juni 25, Harmonize alipiga hatua ya kuomba ndoa na Kajala, takriban miezi miwili tu baada yao kurudiana. Mwezi uliopita staa huyo wa Bongo alimhakikishia ndoa mchumba huyo wake wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Harmonize alimwambia Kajala kwamba kumfanya meneja wa kazi zake za kimuziki ni ishara tosha kuonesha kiasi gani anamkubali, kumuamini na kumpenda bila kujali maneno ya watu kuhusu tofauti kati ya umri wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live