Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala afuta picha za Harmonize

Fb7f563da1211f19c9f1b3c54d42d022 Kajala afuta picha za Harmonize

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAARIFA mitandaoni zinasema msanii wa filamu Kajala Masanja na msanii wa muziki Rajab Abdul ‘Harmonize’ zinasema penzi lao limefika mwisho baada ya Kajala kufuta picha zote kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kajala alifuta picha zote alizowahi kuchapisha akiwa na Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kisha kuacha kuwa mfuasi wake kwenye mtandao na kuandika ujumbe wa lugha ya kiingereza uliotafsirika kama ifuatavyo:

"Usimuumize mtu kwa ajili ya sababu zako binafsi".

Mahusiano ya Harmonize na Kajala yalikuja kwa kasi Februari mwaka huu na yalivutia watu wengi hadi kila mmoja akachora tattoo japo baadhi ya watu wengine walikuwa wakipinga penzi hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz