Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala afunguka kum-cheat Harmonize

Kajala Na Harmonize New Kajala afunguka kum-cheat Harmonize

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja amefunguka kuhusu yanayoendelea mitandaoni kumuhusu yeye na EX waka Harmonize.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Kajala pia amesema kuwa Harmonize ana mazuri yake na mabaya yake kama alivyo yeye Kajala na wanadamu wengine wote.

“Nimepungua kwa sababu Harmonize ni mwanaume wa kwanza maishani mwangu au? Sio kweli, mimi nimepungua kwa sababu ninafanya sana mazoezi, sioni kama nimetikisika kwa kuachana naye.

“Katika mahusiano siku zote hakuna mtu anafanya mabaya tu, hafanyi mazuri, mimi kuna mazuri yangu na mabaya yangu nay eye kuna mazuri yake na mabaya yake.

“Stori ambazo zilikuwa zinaulizwa muda wote ni kuhusu Paula na ndiyo tulikuwa tunzungumzia kwa sabau ilikuwa public na ilishawahi kutupeleka polisi, lakini vile ambavyo ni private sijawahi kuvizungumza na hamna mtu yeyote anayetaka kumuongelea.

“Yeye aje aseme kama alinifumania au nilim-cheat, aseme. Kama aliweza kuandika vitu vingine kwa nini hilo asiseme,” amesema Kajala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live