Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala: Usimuamini Kiumbe Anaitwa Rafiki

KAJALA MWENYEWE.png Kajala: Usimuamini Kiumbe Anaitwa Rafiki

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMAMA Kajala Masanja na staa wa Bongo Movies ambaye haamini katika kuwa na marafiki ambao utawaeleza kila jambo lako na ukabaki salama.

Kajala au Mama Pau ambaye ni mama wa mrembo Paula Kajala anasema watu ambao watu huwaamini na kuwaita marafiki wa dhati, ndiyo hao ambao wamesababisha kuwapotezea ndoto zao, heshima, tabia njema, ndoa na furaha.

Hata hivyo, Kajala anasema kuwa, namna pekee ya kuepukana na jambo hilo ni kuacha kuwaamini watu unaowaita marafiki wa dhati.

“Kuna watu wamepoteza ndoto zao kwa sababu ya marafiki. Kuna watu siri zao zipo hadharani kwa sababu ya marafiki. Kuna watu wamepoteza wapenzi waliokuwa na malengo nao kwa sababu ya marafiki.

"Kuna watu wamekuwa na tabia za ovyo kwa sababu ya marafiki. Kuna watu wamepoteza ndoa zao kwa sababu ya marafiki. Usimuamini sana kiumbe ambaye anaitwa rafiki,” anasema Kajala ambaye mwaka jana alitengana na mpenzi wake, Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live