Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala: Sijauza Range la Harmonize

Kajala Harmo Hj Kajala: Sijauza Range la Harmonize

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja amefunguka kuhusu yanayoendelea mitandaoni kumuhusu yeye na EX waka Harmonize ambapo amekiri kwamba ni kweli miezi miwili kabla hajaachana alikuwa akichukua 10% kutoka kwenye kila hela aliyokuwa akiingiza Harmonize.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Kajala pia amethibitisha madai ya Harmonize kumpa msaada Baba yake Mzazi ambapo amesema ni kweli lakini amekanusha madai kwamba ameuza Range aliyopewa na Harmo.

"Yeye alianza kutumia gari gani kabla ya kuanza kutumia Toyota? Kwa nini tunakuwa washamba na Range? Range sijaiuza, ipo.

"Kuhusu kutumia Toyota mara nyingi mimi natumia gari ya Paula kwa sababu najihisi comfortable zaidi kuliko gari yangu ambayo ina jina, kuna sehemu sitaki watu wajue nipo, hata kama ningetumia IST ni gari," amesema Kajala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live