Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala: Nitakupenda milele Harmonize wangu

Harmonize Kajala   Kajala: Nitakupenda milele Harmonize wangu

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni furaha kwa mwanamuziki na staa wwa bongo Harmonize baada ya mwigizaji na mpenzi wake Fridah Kajali kukubali pete yake ya uchumba.

Hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi ambapo ilihudhuiwa na marafiki, familia na watu mashuhuri.

Wapenzi hao wamekuwa wakivuma mitanddaoni kwa miezi sasa, ii ni baada ya Harmonize kujitokeza hadharani na kuamua kumuomba Kajala msamaha kwa kumkosea.

Harmonize alijaribu vyovyote awezavyo ili kupokea msamaha wa Kajala, na hatimaye aliweza kumsamehe.

Baada ya kumsamehe wawili hao wameonekana kujivinjari pamoja huku mapenzi yao yakionekana kunoga kila siku.

Kajala alimpa ahadi msanii Harmonize baada ya kumvisha pete ya uchumba na kusema kuwa; "Rajabu... Nitakupenda Leo, Kesho, Hadi Milele,"Alisema Kajala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live