Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala: Nina miaka 40 kama 29 tu!

Kajala 29 Kajala Masanja.

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Movies, Kajala Masanja amewajibu wanaomzodoa kuwa amezeeka hivyo abadilike na kujiweka kama mtu mzima.

Ikiwa ni kunbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, Kajala kupitia ukurasa wake wa Instagram amejibu tena kwa shombo akisema; "Maisha yangu ni ya furaha zaidi kuliko vile ningeweza kueleza kwenye umri huu.

"Nina furaha kwamba nilizaliwa kama mimi YES kama mimi na siyo mtu mwingine. Nimekomaa vya kutosha kutambua kuwa mimi bado mtoto.

"Najua safari bado ni ndefu ila Mwenyezi MUNGU atanifikisha tena kwa ushindi mkubwa. Ahsante Mungu wangu, Ahsante wazazi wangu. Heri ya siku ya kuzaliwa kwa toleo bora la mimi mwenyewe.

:NB: 40 is fine when you look like 29. Msinilete makasiriko in this post tafadhali," amesema Kajala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live