Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala: Ni kweli nilikuwa na password ya ATM Card ya Harmonize

Kajala Harmo Kl.png Kajala na Harmonize.

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja amefunguka kuhusu yanayoendelea mitandaoni kumuhusu yeye na EX waka Harmonize ambapo amekiri kwamba alikuwa na password ya ATM Card ya Harmo ambapo alikuwa akichukua pesa.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Kajala pia amethibitisha madai ya Harmonize kumpa msaada Baba yake Mzazi ambapo amesema ni kweli lakini amekanusha madai kwamba ameuza Range aliyopewa na Harmo.

"Suala la password anazosema vijana wake wote wa Konde Gang wana password, kila mtu anatumwa kwenda ATM kumchukulia pesa, kwa hiyo kila mtu ana password ya ATM ya Harmonize. Ukisema ni mimi pekee nilikuwa na paswrod ni kitu cha uongo.

"Kuhusu asilimia 10 wakati tumeanza haikuwa kweli, lakini miezi miwili kabla ya mimi nay eye kuachana ndiyo alinipa hiyo asilimia 10," amesema Kajala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live