Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala, Ndauka ni kama paka na chui

Kajala Ndauka Mz Kajala, Ndauka ni kama paka na chui

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Movies, Kajala Masanja alimfungia milango msanii mwenzake Rose Ndauka tangu aliposema kati ya watu ambao hawezi kuwa na ukaribu nao ni Kajala kwa sababu hana cha kujifunza kwake.

Kauli hiyo ya Ndauka ilitafsiriwa kama dharau ya wazi kwa Kajala na aliitamka kipindi kile wakati Paula akielea kwenye kurasa mbalimbali za mitandaoni baada ya kuhusishwa kutembea kimapenzi na Harmonize ambaye pia alikuwa kwenye mahusiano na mama yake.

Tangu Rose Ndauka atoe kauli hiyo, Kajala alitangaza wazi kuwa hawezi kumkaribisha Ndauka malangoni kwake na hata kwenye shughuli zake za msingi Ndauka hatahusika.

Wiki iliyopita Kajala alikuwa na shughuli ya Babyshower ya Paula na Marioo, kwenye shughuli hiyo walikuwepo mastaa karibia wote lakini Rose Ndauka hakuwepo na hii inaonyesha bado Kajala kamfungia milango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live