Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kajala, Harmonize wamsapraiz Paula

Wasafifm~p~Cg5LozUsuBq~3 Kajala, Harmonize wamsapraiz Paula

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mzazi na baba wa kufikia wa Paula, Kajala Masanja na Rajabu Abdul 'Harmonize' wamemsapraiz mtoto wao kwa kutokelezea kwenye uzinduzi wa duka lake jipya la mavazi aliloliita Paula Closet.

Mchongo huo umechukua nafasi usiku wa kuamkia leo ambapo Kajala na Harmonize waliibuka kwenye duka hilo lililopo maeneo ya Mlimani Driving jijini Dar na kisha kuondoka kabla shughuli haijaisha.

Wawili hao hawakuweza kukaa sana kwa kuwa walikuwa wametokea safari lakini Paula aliwashukuru wote kwa kufika.

Duka hilo ambalo Paula anasema limemgharimu takriban shilingi Mil. 500, amesema fedha hizo amedunduliza kutoka kwenye madili mbambali ya ubalozi aliyokuwa anayapata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live