Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KAUMBA nilikuwa nafanya na Nameless sio Vanessa – Damian Soul

1287 Damian Soul TZW

Mon, 15 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mwanamuziki Damian Soul amesema kolabo yake na Vanessa Mdee ‘Kaumba’ mwanzoni alikuwa amepanga kufanya na muimbaji kutoka nchini Kenya, Nameless.



Nameless, Vanessa Mdee na Damian Soul

Mwanamuziki Damian Soul amesema kolabo yake na Vanessa Mdee ‘Kaumba’ mwanzoni alikuwa amepanga kufanya na muimbaji kutoka nchini Kenya, Nameless.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Data’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa ngoma hiyo mwanzoni aliifanya nchini Kenya mwaka juzi alipoenda kwa ajili ya media tour ambako alishirikina na Nameless studio kwa producer Sappy.

“Ile Kaumba nilikuwa nafanya mimi na Nameless sio na Vanessa, mpaka hiyo vibe inatengenezwa nipo na yeye (Nameless) kuanzia mwanzo, amechangia vitu vikubwa sana mpaka hiyo beat ikaisha,” amesema Damian Soul.

Ameendelea kwa kusema katika muendelezo wa ngoma hiyo ili kuimalizia Nameless alikuwa muda mwingi amebanwa na shughuli zake binafsi hivyo akamuomba aimalizia na msanii mwingine ambaye ni Vanessa.

“Nilimuomba ruhusa, nikamwaambia kaka umefika wakati wa wimbo mimi kuutoa na kama hatojali naweza kufanya na artist fulani akaniambia all the best,” ameongeza.

Ukimuweka pembeni Vanessa Mdee, Damian Soul ameweza kuwashirikisha wasanii kama Joh Makini, G Nako, Nikki wa Pili, Quick Rocka, Banana Zorro na wengineo katika ngoma zake.

Chanzo: bongo5.com