Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KAJALA - Nimeumizwa sana, Hamisa Mobetto alimchukua saa 6

Screenshot 2021 02 14 At 14.59.33 660x400.png KAJALA - Nimeumizwa sana, Hamisa Mobetto alimchukua saa 6

Mon, 15 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

“Mimi ni mzazi ambaye namlea mtoto wangu kwa katika mazingira magumu sana kutokana na tofauti moja mbili tatu na baba mtoto wangu lakini mimi nilikuwa nikipambana na kumpa kila anachotaka mtoto wangu ili aweze kutimiza ndoto zake kama msichana mana kesho nitakuja kumtegemea”

“Nilikua nikikumbana na changamoto tofauti tofauti ambazo zinamkumba paula kama msichana lakini shutuma nyingine huwa zinanijia mimi direct kama mzazi wa paula sina budi ya kuzipokea na kukumbana nazo as long as Mungu anajua ukweli wangu ,jinsi gani namtunza mwanangu na kiasi gani napambana kwa ajili ya mwanangu”

“Yote yaliyotokea ya kunichafua na kunifanya nionekane mbaya kwenye jamii huwa namwachiaga Mungu tu, ilikua tarehe 9 saa 6 mchana hamisa mobeto aliniomba kutoka lunch na mwanangu, sikuona haja kumkatalia kwa sababu nilijua yeye ni mzazi ambaye ana mtoto pia wa kike,kumbe ndo hiyo siku alitake advantage kwenda kumkutanisha na rayvanny kwa manufaa yake binafsi,walimrubuni mtoto mdogo kwa kumnywesha pombe”



“Wamemrekodi video Chafu sawa mimi ni Mnyonge siwezi wafanya chochote basi hata muogopeni Mungu Kama Mungu Hamumuoni Hamuiogopi serikali ? na kuvujisha video bila woga wakati ni mtoto mdogo anasubiria mwezi wa 6 kuingia form 5 siamini kama kuna alie juu ya sheria Katika taifa hili kama leongo lilikuwa ni Kudet Mtoto Mdogo ili Kutimiza Matendo Haya Machu Ya Kustaajabisha haitoshi mnampatia mtoto pombe na kumrecord Video chafu lengo lilikuwa nini Kama sio kuharibu Maisha ya msichana wa kitanzania?”



“Nimeumizwa mno na Hamissa mzazi mwenzangu hata kama iwe paula ndo alimwambia anaenda kukutana na rayvanny kama yeye mzazi ange Vaa kiatu changu na kujiuliza kinachoenda kutokea ni kitu gani au kama ni mimi nafanyiwa hivi ningejisikiaje? nimeshikwa na bumbuazi sina nguvu naomba Mamlaka husika wanisaidie kwenye hili mana hili pigo ni lawazazi Wote Duniani”

“Paula ni msichana mdogo sana ana ndoto zake leo hii ameharibiwa profile nzima Je mmefikiria maamuzi gani anaweza chukua huyu mtoto kuona video kama hizi zinatambaa mtandaoni kama akiamua kujinyonga je? naomba sana msaada serikali yangu na mamlaka husika juu ya hili” ameandika Mwigizaji Kajala Masanja. 

EXCLUSIVE INTERVIEW: P FUNK AKIONGEA KUHUSU MAISHA YAKE, KUTOPENDA KAJALA ANAVYOMLEA MTOTO WAO PAULA, BONGO RECORDS ENZI HIZO NA MENGINE
Chanzo: millardayo.com