Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jux ni nguvu yangu – Mkubwa Fella

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Umekuwa ukiwaza kuwa Jux ni zao la kundi la Wakacha? Basi umekosea sana, nikufahamishe kuwa msanii huyo ni zao la Mkubwa Fella.



Hilo amethibitisha Fella mwenyewe wakati akiongea katika sherehe za uzinduzi wa kumtambulisha msanii mpya wa WCB, Malomboso zilizofanyika Hyatt Regency zamani Kilimanjaro Hotel.

“Mimi na kumbukumbu zangu nimewatengeneza wasanii 105, wanaofanya vizuri 32. Na nitakupeni maajabu mtu mwingine anayefanya vizuri ni Jux ni nguvu yangu. Hamjui mmeona, na sitaki mujue,” amesema Fella.

Mkubwa Fella ameongeza kuwa japo Malomboso amesaini lebo ya WCB lakini bado kuna asilimia atakuwa anaipata kutoka na kumlea msanii huy0 mpaka kuanza kufahamika.

Chanzo: bongo5.com