Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jux ashikwa na kigugumizi kwa Huddah na Vera

JUXMADEMU Jux ashikwa na kigugumizi kwa Huddah na Vera

Mon, 4 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji Jux amesema huwa ni mgumu sana wa kuchagua mwanamke wa kuwa naye kwenye mahusiano na mara nyingi huwa anakuwa na vigezo vingi sana.

Akiongea kwenye Friday Night Live, Jux ameweka wazi kuwa yupo karibu na Huddah kwasababu wameshafanya kazi na wanawasiliana lakini kikazi zaidi.

''Huddah ana mahusiano yake japo mimi kwasasa sipo kwenye mahusiano lakini namheshimu Huddah na hatuna ukaribu huo ila huwa ananipa mawazo ya kazi'' - Jux

Kuhusu kusumbuliwa na wasichana kwenye mitandao ya jamii, Jux amesema inatokea ila sio sana.

Kwa upande mwingine amesema mpenzi wake wa zamani Jackie Cliff, hajawasiliana naye muda mrefu ila anaweza kuwa anakaribia kutoka na kama atatoka wanaweza kuwa kwenye mahusiano ila itategemea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live