Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jux anapogeuka kioo kwa staili zake konki

298 22157789 2015060965392718 2993046903379197952 N TZW

Sun, 17 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Tumemzoea  awapo jukwaani kwa vibao vyake matata na vya kuburudisha hasa vya mapenzi, Juma maarufu kama Jux ameaonyesha umahiri  wake pia katika mitindo na ndiyo maana leo tunamleta kwenu katika stori za mitindo hapa Bongo5.

Unaweza ukamuita mchawi wa mavazi hasa pale anapojaribu kila aina ya mavazi na yanamtoa bomba. Umaarufu katika muziki wake umeenda sanjari na muonekano wake ikiwemo na uvaaji wake tofauti tofauti kila wkati.

Jux ni miongoni mwa wanamuziki Bongo mwenye mashabiki wengi hasa watoto wa kike, hii ni kutokana na kuwa kivutio machoni mwao, mashairi yake pia yamekuwa yakiwabamba  sana na mwisho kabisa ambacho ni kikubwa ni muonekano wake yaani ‘Smart’ kuanzia mavazi, muonekano na haiba yake.

Mkali huyo wa miondoko ya RnB amekuwa kiio kwa jina wengi hasa linapokuja suala la mitupio naweza kusema amekuwa Role Model kwa wakaka wa town wanaopenda kutupia vitu ‘Konki’ lakini pia amekuwa akileta ushindani kwa baadhi ya wabunifu wa mitindo kutamani wamvalishe.

Ukiwa unataka kupendeza tazama wanao kuzunguka.

Chanzo: bongo5.com