Mwimbaji Justin Timberlake alikamatwa mjini New York kwa kuendesha gari akiwa amelewa, maafisa wa eneo hilo wameiambia BBC.
Nyota huyo wa pop alikamatwa na kushtakiwa rasmi Jumanne asubuhi, Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Suffolk ilisema katika taarifa yake.
Timberlake alikuwa Sag Harbour, kijiji tajiri huko Hamptons, mahali maarufu pa majira ya kiangazi kwa watu mashuhuri.
Aliachiliwa bila dhamana baada ya kushtakiwa rasmi, Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Suffolk ilisema.
BBC imewasiliana na wakili wa Timberlake kwa maoni yake.
Timberlake alikamatwa baada ya saa sita usiku polisi walipomvuta kutoka kwa gari lake la kijivu aina ya BMW kwa kuendesha gari licha ya ishara ya kusimama na kushindwa kukaa upande wa kulia wa barabara, kulingana na hati ya mashtaka.
Wakati maafisa walipomsimamisha, macho ya Timberlake yalikuwa "mekundu" na "harufu kali ya kinywaji chenye kileo ilikuwa ikitoka kwenye pumzi yake", hati ya mashtaka ilisema.
Alikuwa akizungumza kwa mwenendo wa pole pole na alifanya vibaya katika majaribio ya kama yuko sawa kwa matumizi ya kileo, maafisa walisema.
Pia alikataa kupumua kwenye kifaa cha kuthibitisha kama amekunya kileo, kulingana na hati ya mashtaka.
"Nilikuwa na Martini na niliwafuata marafiki zangu nyumbani," inadaiwa Timberlake alimwambia afisa aliyemsimamisha, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.
Anatarajiwa kufika katika mahakama ya Sag Harbour tarehe 26 Julai.
Wakili wake, Edward Burke Jr., aliiambia BBC mshirika wa habari wa Marekani CBS Jumanne jioni kwamba "atamtetea mteja wake kwa nguvu zote.
Timberlake, 43, alitarajiwa kuanza ziara ya kimataifa ya albamu yake ya sita, Everything I Thought It Was.